Mke wa T.I ajitetea kubadili macho yake


Mke wa rapa T.I Tameka Harris alitoke kwenye kipindi cha Good Morning America na kueleza namna alivyokwenda Afrika kubadili rangi ya macho yake.
Nyota wa michezo halisi ya runinga (Reality TV) Tameka ‘Tiny’ Harris, mke wa rapa T.I, ametetea uamuzi wake wa kubadilisha kabisa rangi ya macho yake.
Harris, ambaye alikuwa mwanachama wa kundi la miaka 90 la R&B la Xscape, alisafiri mpaka Afrika zaidi ya wiki mbili zilizopita kwa ajili ya kupamba macho ambapo alibadili rangi ya macho yake kutoka hudhurungi (brown) na kuwa na weupe wa barafu (ice grey) – na hakuwa na furaha.
“Nilijitizama kwenye kioo na nilikuwa, kama, yanapendeza,” alisema kwenye kipindi cha Good Morning America siku ya Alhamisi.

Tiny mwenye macho ya hudhurungi akiwa na mumewe T.I Oktoba 3 mjini Atlanta, Georgia.
Alielezea mchakato mzima: “Wanakwenda kwenye jicho na kuyafungua kidogo. Kisha wanachukua kipandikizi na kukiweka juu. Wanakifungua na na kukisambaza juu ya jicho.
“Waliniambia kuwa zoezi hilo lilichukua dakika tano mpaka 10 kwenye jicho. Waliniamsha. Na ilikuwa ngumu kidogo, na kukufanya uanze kuona taratibu.”
Madaktari wamedai kuwa zoezi hilo hufanywa kwa wagonjwa wenye matatizo ya kiafya au masharti.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini