Arsene Wenger: Alexis Sanchez na Luis Suarez ni wapiganaji
Kocha wa
Arsenal Arsene Wenger anasisitiza kuwa upambanaji unaopnyeshwa na Alexis
Sanchez na Luis Suarez umetengenezwa na mitaa ya Amerika Kusini.
Wenger
anahusudu nguvu na bidii ya mchezaji wa Chile Sanchez, ambaye Gunners
walimsajili msimu huu kwa ada ya pauni milioni 35 kutoka Barcelona.
Mfaransa huyo
anaamini utawala wa washambuliaji wa Latini Amerika katika soka la Ulaya
ni matokeo ya malengo wanayohitaji kuyafanikisha katika nchi zao, huku
mataifa yaliyoendelea wamekuwa laini.
“Tazama Ulaya nzima ni wapi wanatoka washambuliaji? Wengi wao, karibia asilimia 80, wanatoka Amerika ya Kusini,” alisema Wenger.
“Labda kwa sababu soka la mitaani Ulaya limekufa. Soka la mtaani, ukiwa na miaka 10, unataka kuja kucheza ukiwa na miaka 15.
“Kisha unatakiwa kudhihirisha kuwa umzuri, unapambana na kushinda mipira isiyowezekana.
“Lakini si kila Mmarekani wa kusini ana hilo, ukirudi miaka 30 au 40 nyuma nchini England, maisha yalikuwa magumu.
“Ila kwa sasa
jamii imebadilika. Tumekuwa watu wa kujihami zaidi ya ilivyokuwa miaka
20 au 30 iliyopita. Tumekuwa walaini kidogo.
“Ukiona mahali wanakotoka, mahali alipozaliwa, na kasha anacheza Barcelona au Arsenal, lazima awe na kitu maalum.