Mauzauza: Fisi wanaswa na shanga na Rozari kiunoni baada ya msako mkali wa wananchi huko Kwimba Jijini Mwanza.
MSAKO
wa Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa
Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.
Maajabu
hayo yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya
12 waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.
Msako Mkali
Msako
huo wasiku tatu ulioanza juzi (Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi
wa Kijiji hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na
Mwang’ombe, wanaotumia siraha za jadi na mbwa wapatao 50.
Habari
za ndani kutoka Kijijini humo zimesema kwamba, kabla ya wananchi hao
kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi wanadaiwa kumilikiwa na
watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina, wazee wa Kijiji
na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na nguvu
za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.
Wazee wanena
Kwa
mujibu wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho ambao hawakutaka majina yao
yaandikwe, walisema kuwa makamanda wa jadi wanaoongoza msakao huo pamoja
na mbwa wao, wana kinga za kupambana na imani za kishirikina vinginevyo
wasingeweza kuua fisi wenye shanga na Rozali wanaotumiwa kishirikina.
Diwani
wa Kata ya Hungumalwa Shija Malando akizungumza na waandishi katika
Kijiji hicho jana, alisema wananchi walifikia maamzi ya kufanya msako
huo wa siku tatu, baada ya kundi kubwa la Fisi hao wanaokadiliwa kuwa
zaidi ya eighty, kuwa tishio kwa watoto na mifugo.
Alisema
kuwa, kwa muda wa miaka miwili iliyopita hadi sasa, licha ya wanyama
hao kuharibu hekali moja ya matunda aina ya Tikiti Maji yaliyokuwa
yamelimwa na mwanchi mmoja, wameua ng’ombe 109, Mbuzi a hundred thirty
five, kondoo 127 na Nguruwe 15 katika Vitongoji hivyo.
“Njooni muone maajabu haya.” Alisema Malando na kufafanua “Jana
(juzi Jumapili) wananchi walifanikiwa kuua fisi kumi wawili kati yao
wakiwa na maajabu. Mmoja aliukuwa na Rozali kiunoni na mwingine akiwa na
shanga kiunoni huku uume wake ukiwa umetahiriwa kama binaadam.”
Alisema
fisi waliokutwa na vitu hivyo kiunoni, kwa imani za kabila la Kisukuma,
wanadaiwa kumilikiwa na baadhi ya watu wenye imani za kishirikina na
kwamba, waliuawa majira ya saa eight hadi saa 10 mchana kwenye eneo la
mlima wa Mwanzabalemi.
Alifafanua
kuwa, fisi kumi waliuawa (jumapili) siku ya kwanza ya msako huo na
wengine wawili waliuawa jana asubuhi na kwamba maeneo ya milima ya
Mwanangi katika Kijiji cha Buyobo na Kitongoji cha Mwanzabalemi
yanasadikiwa kuwa na fisi wengi zaidi.
“Pamoja
na kushambulia mifugo yetu, ilifika mahali wananchi walikuwa hawawezi
kutembea kwa uhuru nyakati za usiku na baadhi ya watoto wanaosoma mbali
kukatisha masomo kwa kuhofia kuliwa na fisi hao.” Alieleza Mwenyekiti wa Kijiji cha Hungumalwa, Clement Kaswahili.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Mwang’ombe Joseph Kisena alisema hadi kufikia leo
(siku ya tatu ya msako huo) watakuwa wameua fisi wengi zaidi kutokana na
ushirikiano mzuri wa Vitongoji hivyo vinavyotumia mbwa 50 na silaha
mbalimbali za jadi ikiwemo mikuki, mapanga na marungu.
Kisena
alisema, pamoja na maajabu ya fisi kuvaa shanga na Rozali kiunoni
ambayo wamejionea na kuzua imani za ushirikina kwa baadhi ya wananchi,
hawatarudi nyuma, hadi walitokomeze kundi la wanyama hao ambalo ni
tishio kwa wananchi na mifugo yao.
“Njooni muone maajabu haya.” Alisema Malando na kufafanua “Jana
(juzi Jumapili) wananchi walifanikiwa kuua fisi kumi wawili kati yao
wakiwa na maajabu. Mmoja aliukuwa na Rozali kiunoni na mwingine akiwa na
shanga kiunoni huku uume wake ukiwa umetahiriwa kama binaadam.”