Mwigizaji Jack Pentzel na Mumewe Kimenuka

NDOA ndoano! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Steven Pentzel ‘Jack Pentzel’ na mumewe Gardner Dibibi wanadaiwa kukinukisha na kuingia kwenye gogoro la kila siku hadi mwanaume kutaka kuondoka nyumbani wanakoishi Mbezi-Shamba jijini Dar.

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao, kilisema kwamba, kila kukicha wawili hao wamekuwa wakigombana na sababu kubwa ni Jack kuchelewa kurudi nyumbani.

Ilidaiwa kwamba, tangu Jack awe na ushosti na staa mwenzake wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amekuwa ni mtu wa kujiachia na kujisahau kwamba ni mke wa mtu. “Yaani ndoa ya Jack inashikiliwa na uzi kwani kila siku wanapigana na hivi karibuni mumewe alikusanya nguo na kuweka kwenye begi akitaka kuondoka nyumbani.

“Tatizo mwanamke anachelewa kurudi nyumbani, mumewe akimuuliza ndiyo mgogoro unaanzia hapo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka mume wa Jack, Dibibi ili kueleza ukweli juu ya suala hilo.
Credits:Global Publishers

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini