NJIA SABA (7) ZA UHAKIKA ZA KUPATA AJIRA HIZI HAPA
pay per click advertising Kupata nafasi za ajira imekuwa ngumu siku hadi siku, hususani ukitilia maanani kuwa wahitimu wanazidi kuwa wengi na hali ngumu ya uchumi inafanya waajiri kushindwa kuongeza nafasi mpya za kazi. Hauna haja ya kukata tamaa ya kupata kazi ile unayoitarajia hata kama kuna ukiritimba mwingi katika soko la ajira kama vile watu kupeana kazi kwa kujuana, nafasi za kazi kutotangazwa au kazi haipatikani mpaka rushwa itembee. Makala hii inaenda kujadili mambo ya msingi kwa yeyote anayetafuta kazi, uwe kwa sasa umeajiriwa unatafuta kazi mbadala au uwe hauna ajira unatafuta ajira, bila shaka mambo tunayojadili hapa yatakusaidia. 1.Mtazamo wako kuhusu ajira: Fahamu kuwa bidhaa ni chochote kile ambacho kinatimiza mahitaji fulani. Mwenye kuhitaji bidhaa huwa tunamuita mteja . Muajiri anatafuta mfanyakazi kwa kuwa analo hitaji la kazi fulani kukamilika, na anayo matarajio kadhaa toka kwa mfanyakazi anayemuajiri. ...