Wabunge Wenye Miaka 15 na Zaidi Bungeni na Bado Wanataka Kugombea Ubunge 2015

Naomba tuwatambue wabunge ambao wamekuwepo bungeni kwa muda wa miaka 15 na kuendelea na bado wanataka kugombea tena, wa vyama vyote.

Hii itasaidia kuwakumbusha waheshimiwa hawa kujitathmini kwa muda waliowakilisha wananchi na kile kilichopatikana kwa kipindi chake na wajitathmini kwanini waendelee kugombea. Na pia kuepuka miungu watu katika baadhi ya majimbo ambao wamekuwa chanzo cha kuzorota kwa maendeleo majimboni kwao.

Watia nia wengi wa uraisi ni wale waliokaa kipindi kirefu katika nafasi ya ubunge na namna ya kuachana na ubunge ni kugombea urais. Wapo waliokwisha kutangaza kuachia majimbo kama:

Edward Lowassa 20yrs, John Magufuli 20yrs, Samwel Sitta 20yrs, Steven Wassira 20yrs, n.k

Wapo ambao wamekuwa wabunge zaidi ya miaka 15 na hawajasema chochote mfano: Lekule Laizer 20yrs, Hendrew Chenge 20yrs, Wilium Ngeleja 15yrs, Marry Nagu 15yrs, n.k.

Naomba tuwabaini wengine ambao wana muda mrefu kama huo na bado wanautaka ubunge. Taja jina la mbunge, jimbo, muda na kama ameshasema chochote.

Ahsante nawasilisha.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini