Mashabiki Wamvaa IRENE PAUL Baada ya Kutoa Kauli ya Kuudhi ..Wasusia Movie zake


Baada ya siku kadhaa muigizaji irene paul, kupokea Tuzo ya muigizaji bora wa kike mwaka 2015 (TAF) , Msanii huyo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya ivi karibuni kufanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha television ,ambapo aliulizwa swali na mwandishi, ni movie ipi ya kibongo anayoikubali?, ndipo msanii huyo alipofunguka bila kumung'unya maneno kuwa sio muangaliaji wa bongo movie, hivyo hajui chochote. kauli hiyo ilizua tafrani kwa baadhi ya mashabiki zake ambao walimjia juu muigizaji huyo mwenye makeke ya aina yake awapo mbele ya camera.

Baadhi ya Comments 

# 1: Huyu dada anajisikia sana, hajui kuwa sisi ndio tuliomfanya awe mtu, bila kuigiza nani angemjua apa mjini? Sijapenda kauli yake ata kidogo.

# 2: Najuta kabisa kwa nini nilimpigia kura, kama yeye msanii haangalii bongo movie, sasa sisi tuangalie ili iweje? Atakula jeuri yake mwaka huu, hiyo tuzo ndio ya mwisho.

# 3: Kwanza mie sionagi uigizaji wake zaidi ya kupiga kelele ovyo na kujitutumua kama anataka kukata roho, mimi simkubali huyo dada anajisikia sana.

# 4: Kuna siku nilikutana nae mlimani nikamuomba kupiga nae picha akaniambia yeye sio irene Paul nimemfananisha, ata hivyo niliomba tu kupiga nae picha kwa kuwa nilimpenda, jibu alilonipa eti mi msumbufu sana ,yeye yupo busy na mambo yake, kweli anatujibu hivyo mashabiki zake? Nilisikia aibu sana kwa kweli aliniaibisha mbele za watu,sitakaa nimpende.

# 5: Kama haangalii kazi wanazofanya wenzie atajuaje changamoto zilizopo kwenye filamu na kuzifanyia kazi? Kauli yake sio nzuri, kwa hiyo anatuona tunaoangalia kazi zao hatuna akili?

# 6: MUongo mkubwa anajishaua tu, anajifanya anafanana na angelina jolie na mishavu yake kama panya, simpendi huyo dada.

# 7: Mi namkubali sana irene paul, ila hiyo kauli sio nzuri, ata kama ni kweli aangalii ni bora anfefikiria kabla ya kuongea, by the way mi namkubali tu.

#8 : Kwanza hiyo tuzo kapewa kwa uigizaji upi? Mi sijaona anachoigiza zaidi ya kutumia nguvu kuliko akili, kama haangalii bongo movie anaigiza ili iweje? Basi akaigize ulaya

# 9: Huyu dada anajiona mzuri wakati kakomaa kama nazi, kwanza kuigiza hajui, kanichefua sana, tutakua hatuangalii movie zao tuone hizo jeuri watapatia wapi

# 10: KWa hiyo kapata tuzo ndo anajidai kuropoka? Sasa akipata oscar si ndio ataikana kabisa Kuwa yeye sio muigizaji wa Tanzania?

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini