Umri wa Sitti Mtemvu Bado Mzigo Mzito Kwake, Agoma Kata Kata Kutaja Umri wake Sahihi

Miss Tanzania ambaye alilivua taji mwaka jana 2014, Sitti Abass Mtemvu amekiri wazi kuwa maisha yake hayakuwa na amani tena toka skendo yake ya kudanganya umri katika mashindano ya Miss Tanzania, ambapo yeye aliweza kuibuka mshindi na kuvishwa taji hilo, Jana kupitia katika kipindi cha Fashion cha NIRVANA cha EATV, Malkia huyo alionyesha wazi kuwa suala la umri wake bado ni mzigo mzito kwake kwani hakuwa tayari kuweka ukweli kwa jamii juu ya umri wake.

"Naomba watanzania tuachane na suala la umri wangu maana si jambo la msingi sana ila tunaweza kuaangalia mambo mengine ya msingi ya kimaendeleo, maana kwa sasa hilo suala mimi nishalifunga na naangalia mbele mambo mengine ya msingi"

Japo Mtangazaji wa Kipindi cha Nirvana alitumia muda muda mwingi kumbana Sitti kuhusu Umri lakini Sitti hakukubali Kutaja umri wake sahihi ....

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini