AJABU:Mwanaume Apandikiziwa Uso wa Mtu Mwingine Baada ya Uso wake Kuaribika na Kuwekewa Sura ya Mtu aliyekufa

Ajali nyingi duniani zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi huku zikiacha wengine wakiwa na ulemavu wa maisha ambao huwasababishia kupoteza mwelekeo wa maisha yao na kukata tamaa kabisa.
Pamoja na wengi kubaki na ulemavu, lakini pia madaktari wamekuwa kijitahidi kadri wawezavyo kuwarudisha watu hao katika hali zao lakini moja ya tukio la kushangaza ni la kijana Richard Norris ambaye alipata ajali mbaya na kumpelekea kuharibika vibaya sura yake.

Unaambiwa baada ya ajali hiyo kijana huyo alishindwa kutoka nyumbani kwa takribani miaka 15 na amini usiamini kijana huyo alifanyiwa upasuaji wa kihistoria uliochukua masaa 36 na kupandikizwa uso mpya wa mtu ambaye alishafariki baada ya kupata ajali.

Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya University of Maryland Medical Center na ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa na sasa kijana huyo anaendelea vyema akiwa mwenye furaha.

Kwa kawaida kwa sababu ya maadili ya utabibu watu waliopewa mabaki ya viungo vya wafu hawaruhusiwi kukutana na jamaa au ndugu wa marehemu, lakini Norris hakuweza kujizuia kukutana na Aversano, kutoka Maryland ambaye ni dada wa marehemu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini