Lowassa Amtisha Rais Kikwete

EDWARD Lowassa, mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliojiapiza kufia katika urais, amekimega chama hicho vipande viwili. Anaripoti Yusuf Aboud … (endelea).


Lowassa aliyekuwa mmoja wa wanachama sita wa chama hicho walikuwa katika uangalizi, anadaiwa kuwa ameshindikiza kuondolewa mapema adhabu hiyo, vinginevyo angeondoka.

“Ni kweli chama chetu kimemshindwa Lowassa na sasa kimemuondoa kifungoni. Hii maana yeka ni kwamba sasa Lowassa yuko huru kuwa mgombea urais wa chama chetu katika uchaguzi mkuu ujao,” anaeleza mjumbe mmoja wa NEC aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Amesema, “Kwa maoni yangu, hatua hii itakidhoofisha zaidi CCM kuliko kukiimarisha. Kama CCM inajitakia mema, hakiwezi kuruhusu Lowassa kuwa mgombea wake. Huyu mtu amekivuruga chama chetu. Amenunua watu wetu na amekigeuza chama kuwa genge la wanunuzi wa kura.”

Jana Jumatatu, Kamati ya Maadili ya chama hicho iliyodai ilikuwa na “faili la Lowassa na watuhumiwa wengine sita,” imesema kuwa mwanasiasa huyo “hana tena hatia na kwamba adhabu aliyopewa tayari imemalizika.”

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa ndani ya chama hicho wanasema, “kuachiwa huru Lowassa” kunathibitisha udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho, katika kusimamia chama chake.

Taarifa zinasema, ikiwa Lowassa atakapitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake urais, taifa litaendelea kutumbukia katika visa vya visasi, kutekwa na kuteswa, kumwagiwa tindikali na matukio mengine dhidi ya wananchi na vyombo vya habari.

Aidha, watu kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Salma Kikwete, Bernard Membe, George Madafu, Jack Zoka na Othuman Rashid, wataweza kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Wengine wanaoweza kufikishwa mahakamani, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, ambao watatuhumiwa kuandika uchochezi na kudhoofisha serikali.

Jakaya Kikwete ambaye ndiye rais wa Jamhuri, amewahi kunukuliwa na mmoja wa marafiki zake akijiapiza kuwa “Lowassa hawezi hata kufikiriwa kuwa mgombea urais.”

Hivi karibuni, gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki lilichapisha taarifa kuwa Lowassa anaungwa mkono katika mbio zake za kugombea urais na aliyekuwa mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Rostam ametajwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, Col. Apson Mwang’onda ambaye alitajwa kuwa mwenyekiti wa “kamati ya ushindi ya Lowassa.”

Rostam ambaye amehamishia sehemu kubwa za biashara zake nchini Kenya na Dubai kwa sasa, ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa Kikwete katika mbio za urais mwaka 2005.

Mfanyabiashara huyo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Igunga (CCM), alikuwa miongoni mwa kundi lililohodhi CCM na kufanya maamuzi mengi kwa niaba ya chama na serikali. Katika miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Kikwete, Rostam alifanywa mweka hazina wa chama hicho.

Mbali na Rostam Aziz, Lowassa amezunguukwa na watu wengi wanaotiliwa shaka uadilifu wao mbele ya jamii, akiwamo Andrew Chenge na Nazir Karamagi

Source:Mwanahalisionline

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini