Mtoto wa Frolah Mvungi,Tanzanite acheza filamu kama ‘Albino’



Flora Mvungi na Mtoto wake Tanzanite
Mtoto wa msanii wa Bongo Fleva,H: Baba na mwigizaji wa Bongo Movie,Frolah Mvungi,Tanzanite amecheza filamu kama mhusika mkuu.

Akizungumza na Clouds FM,H:Baba alisema kuwa katika filamu hiyo ambayo hajaitaja jina Tanzanite amecheza kama mtoto aliyetekwa na watu waliodhania kuwa mtoto huyo ni mlemavu wa ngozi ‘Albino’.

‘’Mimi na Frolah tumecheza kwenye filamu hiyo na Tanzanite kama mtoto wetu amecheza nafasi nne kwenye filamu hiyo kuna watu wanamteka mtoto wangu wakidhani kuwa ni albino ndiyo maana tulimpaka hina kichwani ili afanane lakini baadaye wanagundua kuwa mtoto huyo siyo albino,’alisema H:Baba.

Hiyo ni filamu ya tatu wasanii hao kumshirikisha mtoto wao chini ya kampuni yao ya Double H Film

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini