Riyama Ajivunia Maneno ya Kiswazi


Staa wa Bongo Movies, Riyama Ally, ameibuka  na kusema anajivunia  kuwa na manenona misemo ya kiswazi  ambayo huzungumzwa na wanawake wanaishi sehemu  za uswahilini ndiyo maana amekuwa akishirikishwa kwenye Filamu nyingi.

Akizungumza  na  Tanuru la Filamu jana, Rayama  alisema  kuwa filamu mpya iitwayo WOGA  ambayo ipo madukani sasa imesababisha watu wengi wahisi kama ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwake kwa sababu uhusika alioubeba  huku unaonekana ndivyo tabia yake.

Nine kila sababu ya kujivunia maneno  machafu  ya uswahilini kwani hayo ndivyo  yananifanya nipate mialiko  mingi ya kuigiza  kama  nilivyoshirikishwa  kwenye filamu  hii ya WOGA ambayo ni mejitahidi  kuuvaa uhusika  na kitendo hiki ndicho kinanipa heshima badala ya kuwa na skendo kama wafanyavyo wasanii wengine" alisema Riyama.

Mbali na Riyama wasanii wengine waliocheza kwenye filamu hiyo inayosambazwa na Freshas Campany Ltd ni David Justine, Hashim Kambi, Abdalla Hamis na Mohamed Fungafunga.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini