Eti wakili Mkenya ataoa mtoto wa Obama?? Ona mipango yake sasa aliyojipanga !!


Kila mtu ana ndoto na mtu ambaye anamhitaji awe mpenzi wake kwa maisha yote, sio ajabu mtu akawa na ndoto za kumuwaza mtu ambaye ni ngumu sana kwenye mazingra ya kawaida kuonana nae, pata picha ya huyu jamaa ambaye yeye macho na akili yake ni kwa Malia Obama.

Kiprono Matagei kazi yake ni wakili Kenya, ndoto yake ni yeye na Malia Obama damdam, alianza kumpenda tangu mwaka 2008.. moyoni mwake akaweka ahadi kwamba hatokuwa na uhusiano na mwanamke yoyote mpaka siku ampate Malia wake !!

Jamaa kajiongeza kabisa, amesema mahari aliyopanga kutoa ni hii>>> ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30.

Kiprono kasema yuko serious kabisa na aliwashirikisha familia yake, wako tayari nao kumsaidia mpaka afanikiwe !!

Obama atakuwa Kenya mwezi wa saba, ziara yake haitachukua muda mrefu lakini jamaa amesema atajitahidi aitumie nafasi hiyo hiyo kumuona ‘baba mkwe huyo mtarajiwa’ !!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini