Vita Dhidi ya Diamond ni Kubwa Kuliko Tunavyofikiria


Hakuna ubishi kua kwa sasa diamond platnumz ndie msanii anae ongoza kupigwa vita kuliko msanii yeyote hapa nchini.
Vita hiyo ina ongozwa na baadhi ya walio wahi kuwa wapenzi wake pia na mahasimu wake wa kimuziki (wasanii wengine) kupitia mashabiki zao.
Sawa ni jambo la kawaida kwa wasanii wakubwa duniani na mastar wengine kama wachezaji,maboxer pamoja na waigizaji kuwa na maadui hili linathibitishwa na mfano wasanii kadhaa wa kimarekani walivyo na maadui mpaka inafikia kupigana risasi mfano 2pac,BIG,50cent,mayweather na wengine kibao.

Sababu kubwa za diamond kuanzishiwa vita "maalum" ili ashuke kimuziki na kimafanikio ni kutokana na maneno ya wengi eti kua anaringa,anadharau,ana nyodo,ana mamneno ya shombo,ana ropoka sana,mtoto wa uswahili,hajasoma,mchawi na visababu kedekede.
Wadadisi wa mambo wanasema kua chuki dhidi ya diamond si tu inatokana na sababu zilizo tajwa hapo juu bali inaenda mbali zaidi mapaka kwa team nzima ya diamond hasa mameneja wake.
hapa ni kwamba kwa sasa hakuna asie jua kua unapo ongelea mameneja wakali Tanzania una waongelea Babu tale na Said Fella,Mzozo unakuja pale ambapo kuna watu wanatamani kufika level za wakina Tale but wana chemka ndipo wanapo anzisha kampeni ya kuwaharibia hawa jamaa kwa kisingizio cha kua eti ni wanyonyaji,wana haribu soko la muziki wa bongo fleva na maneno kibao.
kiukweli hawa watu hawajawahi kushindwa kwenye menejimenti yao,kila msanii wanae mmeneji lazma afike mbali wangapi wamejaribu wakaishia njiani? mfano ustadh "juma na musoma", 
Kwa hiyo tunapo itizama vita dhidi ya diamond tusidhani tu kua mashabiki ndio wanao tengeneza hii chuki bali ni mkono wa wadau wakubwa wa muziki hapa nchini wakishirikiana na media kadhaa kuhakikisha wana wapasua mashabiki kwa makusudi tu ili watimize malengo ya kuwamaliza wahasimu wao diamond Fella na babu Tale...!!
Tupingane kwa hoja na sio matusi!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini