MIZENGWE Mtoto wa Aunty Ezekiel, Wadai Afanani Hata Kidogo na Moses Iyobo, Aunty Abanwa, Alichokisema Hichi Hapa



Aunty Ezekiel Akiwa na Mwanaye Cookie Ambae Amezaa na Moses Iyobo Mcheza Dansi wa Diamond
Mtoto wa kike wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson aliyejifungua mwishoni mwa wiki iliyopita na kumpa jina la Cookie (keki ndogo lakini tamu) anaanza kung’aa kwenye vyombo vya habari baada ya baadhi ya watu kumpiga zengwe la madai kwamba eti hafanani na baba yake, Moses Iyobo ‘Moze’.

Huku ishu hiyo ikipingwa vikali na Aunt, washakunaku wa mambo ya watu waliozungumza na Amani  baada ya kumuona Cookie walidai kwamba mtoto ni mweupe wakati Moze ni mweusi ‘tiii’.Zengwe hilo lilianza kusambaa miongoni mwa mashosti waliokwenda kumpa hongera Aunt nyumbani kwake, Kinondoni, Dar, saa chache baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Unajua tangu akiwa mjamzito kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona mtoto kujua kama kweli ni wa Moze maana mwanzoni hakuna aliyeamini kama mimba ni ya Moze ‘so’ hao ndiyo wameanza chokochoko,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutochorwa gazetini.

Baada ya kunasa zengwe hilo, Amani lilimtafuta Aunt ili azungumzie ishu hiyo ambapo alifunguka;
Amani: Kuna zengwe juu ya baba wa mtoto wako, kwani mwanao anaitwa nani?
Aunt: Anaitwa Cookie Lapri-Center.

Amani: Yaani Lapri-Center ndiyo jina la ukoo?
Aunt: Mambo mengine hayawahusu. Mnataka jina la ukoo la nini?
Amani: Watu wanauliza, wanataka kujua maana tayari kuna zengwe juu ya baba wa mtoto.
Aunt: Acheni mambo yenu (kisha akakata simu).

Aidha, madai kutoka kwa chanzo chetu ni kwamba baada ya kuibuka kwa zengwe hilo, Aunt ameamua kumficha mtoto wake.

Source:Gazeti la Amani

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini