ARSENAL YATWAA KOMBE LA FA KWA KUICHAPA ASTON VILLA 4-0


Mabingwa mara 12 wa Kombe la FA, Arsenal baada ya ushindi wa leo dhidi ya Aston Villa.
Arsenal wakisherehekea ubingwa wao wa FA.
Theo Walcott akiifungia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 40.

Walcott akishangilia bao hilo.
Alexis Sanchez (kushoto) akipiga shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Arsenal bao la pili.
Per Mertesacker akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la tatu kwa Arsenal.
Olivier Giroud akifanya hitimisho kwa kutupia kambani bao la nne.
ARSENAL imetwaa Kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley usiku huu.
Mabao ya ushindi ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika ya 40, Alexis Sanchez dakika ya 50, Per Mertesacker dakika ya 61 na Olivier Giroud aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao dakika ya 90.
Kwa matokeo ya leo, Arsenal wameweka rekodi ya kulichukua kombe hilo mara nyingi kuliko timu nyingine yoyote wakiwa wamelitwaa mara 12.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini