Linex:Sijui Nani Gundu Gani Kila Nikiachana na Mwanamke Anakuwa Adui Yangu

 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’, amesema tangu ameanza kujihusisha katika mapenzi hajawahi kuachana na mwanamke yeyote bila ya kuwa maadui.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Linex alisema haoni sababu ya kuwa hivyo kwasababu hakuzaliwa pamoja na mwanamke huyo lakini anashangaa imekuwa ikimtokea hivyo.

Alisema ni vizuri kumfanya mpenzi wako wa zamani awe rafiki yako wa karibu ili kuweza kubadilishana mawazo na sio kununiana kuwa kama paka na panya.

Ukweli toka nimejua kumpenda mtoto wa kike au kuwa kwenye uhusiano sijawahi kuachana na mtu alafu mahusiano yanapokwisha yule mtu asiwe adui yangu,” alisema.

Sijawahi kujua uzuri wa kumfanya mpenzi wangu wa zamani awe rafiki yangu wa karibu ninachomaanisha ni kuwa hatukuzaliwa pamoja na leo hatuko pamoja basi sitaki kuwa na uadui na wadada ambao nishawahi kuwa na uhusiano nao tuwe marafiki ,” alisema Linex.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini