Utambulisho mpya wa Jiji la Dar es Salaam Kwa Sasa...Majengo Mapya na Marefu Yaibuka Kila Siku

Jiji la Dar es Salaam linakuwa kwa kasi kubwa,
Miaka ya zamani jiji hili lilikuwa linatambulishwa kwa kuona picha ya ghorofa la kitega uchumi (ukiachilia mbali mnara wa askari), baadae yakajengwa majengo mengine marefu na jengo la kitega uchumi likafunikwa, likaja jengo la Benjamin Mkapa Tower, (Zamani mafuta house), na sasa zama za jengo la benjamin mkapa tower pamoja na PPF tower zimeshapita, na kwa sasa utambulisho mpya ni haya majengo yaliyopo jirani, ghorofa la PSPF pamoja na ghorofa la One Bandari tower ambayo yote yapo Sokoine drive.

Hii ni tofauti na jiji la Nairobi ambalo miaka nenda miaka rudi limekuwa likitambulishwa kwa picha za jengo la kituo cha mikutano cha Kenyatta.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini