BET walitulipa milioni 46 kwa kucheza video ya Diamond kwa siku 4 tu – Babu Tale

Amini usiamini Diamond Platnmuz alifaidika mara mbili baada ya video yake kuchezwa na kituo kikubwa cha runinga cha Marekani, Black Entertainment Television (BET) mwaka jana.

Faida ya kwanza ni yeye kama msanii wa Bongo flevah kupata nafasi ya video yake kuchezwa na kituo hicho kikubwa cha Marekani, na faida ya pili ni kulipwa pesa nyingi kwa video yake kuoneshwa kupitia kituo hicho.

Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kuwa BET iliwalipa shilingi za kitanzania milioni 46 kwa video ya Diamond kuchezwa kwa siku nne tu na kituo hicho.

kwenye siku nne tukalipwa milioni 46, siku nne kwasababu nyimbo yake imeonekana kwenye TV,”. Tale aliiambia Amplifaya ya Clouds FM.

Ameongeza kuwa BET walielekeza jinsi mgao wa pesa hiyo ulivyotakiwa kufanywa kwa wote waliohusika katika kazi hiyo.

lakini walituonesha hii hela inaenda kwa huyu hii hela inaenda kwa huyu, kwa producer, kwa director, kwa editor, ya msanii ilikuwa milioni 19 kitu kama hicho. Hatukua tumeamini, mimi nimetumiwa e-mail ebwana wasije kuwa matapeli wanataka kuhack wale, kuna hela yetu tufanye process watu watuwekee kwenye akaunti…kuchunguza file ya kuonesha ngoma imepigwa BET four days, media za wenzetu zinalipa vizuri.” alimaliza Tale.

Mwaka 2014 Diamond alitajwa kuwania tuzo za BET kwenye kipengele cha ‘Best International Act: Africa’ akiwa msanii pekee wa Afrika Mashariki, lakini hata hivyo Davido ndiye aliibuka mshindi wa kipengele hicho.

Bongo5

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini