Nimeshatoa Mimba Nyingi Sana-Irene Paul

Muigizaji wa filamu za kibongo ambaye wiki iliyopita ameshinda tuzo ya muingizaji bora wa kike katika tuzo za Filamu nchini Tanzania (TAFA) Irene Paul amefunguka na kusema kuwa
ameshatoa mimba nyingi sana, Irene Paul alisema hayo alipokuwa akichat Live katika kipengele cha KIKAANGONI kinachofanyika katika ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka kumi Alasiri.
Irene Paul alisema kuwa mara nyingi amekuwa akitoa mimba hizo katika filamu kutokana na kuuvaa uhusika ili kufikisha ujumbe kwa jamii kama ambavyo Scene inamtaka kufanya hivyo, lakini katika uhalisia hajawahi kufanya jambo hilo.

"Irene Bahati Paul, katika movie nimetoa mimba nyingi sana maana ndivyo uhusika umenipasa kufanya hivyo ili kuwasilisha ujumbe katika jamii ila kiuhalisia sijawahi kufanya hivyo."
Lakini pia Irene Paul alizidi kuwachanganya mashabiki alipoulizwa juu ya kuwa ana watoto wa ngapi na kusema kuwa ana watoto wengi sana hali ambayo ilifanya mashabiki kutaka kujua watoto wengi kiaje na ni wanani na hapo ndipo aliposema kuwa, yeye hata watoto ambao amewasaidia kuwalea anawahesabu kama ni watoto wake, maana wamepata malezi yake na wao wanamchukulia kama Mama yao.

" Watoto nilionao wengi sana mpenzi, kuanzia niko shule nilikuwa na adopt watoto kishuleshule, na wale wote ninaowasaidia kwa njia moja au nyingine wananichukulia kama Mama maana mimi ni mlezi wao."

Irene Paul ambaye kwa sasa anaonekana kukubalika kutokana na ufanisi wake katika kazi yake ya sanaa alisema kuwa katika maisha ya mahusiano na mapenzi amekutana na changamoto mbalimbali hususani kama kutendwa sababu na yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, kwa sasa adai hajaolewa na kuongeza kuwa kwa wakati huu wa sasa hafikiri kutafuta Mume wala mchumba ila anajipanga tu kusambaza kazi zake tofauti na sanaa.

" Mimi ni kama binadamu wengine napitia yote kama mwanadamu mwingine wa kawaida katika maisha, kwa sasa jibu langu ni sitafuti mume wala mchumba najitayarisha kusambaza kazi yangu tofauti na sanaa, kisanaa najipanga kutoka katika ubora zaidi maana baada ya kuona mapokezi na apreciation za watanzznia nadhani wananidai zaidi ya ninavyowapa".
Ukiachia mbali juu ya sanaa yake Iren Paul amesema kuwa anatamani kuona yeye amekuja daraja ambapo watu watamkumbuka kwa mchango wake wa mawazo, maneno au vitendo hata kimali ili mradi tu atumike katika kufanya jambo hilo.
"Katika maisha yangu yajayo natamani kuwa daraja ambalo siku moja mtu atalikumbuka na kusema ni kwa sababu ya lile au yule nimefika nitakako yaani iwe kwa mawazo maneno au vitendo, kihali au kimali ili mradi tu nitumike"

Lakini pia muigizaji huyo wa bongo movie alimaliza kwa kutoa darasa kwa baaadhi ya watu wanaohitaji kujiunga katika tasnia ya filamu Tanzania na kuwaambia kuwa kila jambo linahitaji malengo na mipango huku ukitambua unafanya nini lakini akadai atatoa darasa kupitia semina mbalimbali atakazoandaa ili kuwasaidia watu wanaohitaji kuingia katika tasnia hiyo.
"Nitawapa semina mbalimbali kupitia mikutano midogomidogo nItakayoiandaa hivi karibuni na kutembelea shule mbalimbali kuwatia moyo wale wenye nia ya kufika mbali lakini kwa wale ambao wanahitaji kujiunga katika tasnia kwanza jua unataka uigizaji kwa sababu gani,halafu weka malengo yako na uyaamini kwa kuyatekeleza,njia ni kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha unaifanya kwa ubora pale upatapo nafasi ,thamini kidogo ulichonacho maana kupitia hicho utapata kikubwa utakacho"

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini