Updates toka Arusha: Mkutano wa Lowassa wa Kutangaza nia ya Kugombea Urais leo


Leo ndio ile siku tuliyokuwa tukiisubiria kwa hamu, Siku ya maajabu, Siku ya mazingaumbwe, Siku ya kuzuiya mafuriko kwa mikono, Siku ya kufanya bishara bila mahesabu, Siku ya kutuza Fedha bila Daftari.

Kwa heshima na taadhima mwanahabari wenu toka chombo cha habari cha kwaminika, chombo kinachofanya kazi bila kupokea bahasha, chombo kilichobaguliwa na mafisadi, Chombo kinachotoa ruhusa kwa kila members kukusanya na kurusha habari, Chombo chenye herufi mbili "JF" kambanda wa ukweli nipo hapa stadium nikishuhudia mazingaumbwe.

Tokea jana nilikuwa nikirandaranda kwenye mitaa na chocho zote za jiji la harusha lakini sikukutana na pikipiki, baisikeli, ng'ombe, mbuzi au gari la matangazo ya mkutano wa leo.

Leo pia nimeamka saa 10 alfajiri/usiku kuendelea kutafuta ata fisi au nguchiro akitangaza mkutano wa Ngoyai lakini nimeambulia patupu.

Muda huu nimeamua nijikite hapa Shekhi Amri Abeidi Karume na kamera zangu ili nipate picha za mazingaumbwe ya leo. Kiukweli uwanja umependeza sana majukwaa yapo matatu sijui ni tamasha la Fiesta? na sound system iliyofungwa hapa siyo ya kitoto na sijui huyu jamaa kaitoa wapi?

Mandugu kaeni mkaowa kula...............

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini