Dudu Baya kurudi rasmi kwenye muziki kwa jina jipya, ‘Dudu Mamba’

Msanii wa Hip Hop wa muda mrefu, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amedai kujipanga kurejea rasmi kwenye muziki wa Hip Hop na kuahidi kuweka ushindani mkubwa na wasanii wenzake wakiwemo Fid Q na Young Killer Msodoki.

Dudu Baya ameimbia Bongo5 kuwa si kwamba anarudi na muziki mpya tu bali pia akiwa na jina jipya – Dudu Mamba.

“Ushindani nitauweza najua kuna wasanii kama Fid Q, Young Killer na wengine wanafanya vizuri lakini mimi sasa hivi nimekuja kushindana,” amesema Dudu Mamba.

“Unajua hii miaka miwili nilionekana kutokuwa serious na muziki lakini sasa hivi tayari nimeshaingia studio za Mona Gangster. Mona ndo kamtoa Young Killer ngoma zote na wasanii wengine, kwahiyo tayari silaha ya kwanza katika kurudi kwangu ni kufanya kazi katika studio bora chini ya producer bora Mona Gangstar.

Silaha ya pili ni mpangilio wa promotion ya ngoma yangu mpya. Nimeshazungumza na wadau mbalimbali wa media kuangalia jinsi gani tunawezafanya kazi kwa kushirikiana, kwahiyo matumani ya kurudi katika level zangu yapo. Ngoma yangu inaitwa ‘Kuwachora kwa Jicho’ ngoma ambayo natumani itakuwa poa sana kwa sababu ngoma ni ya kuchezeka.”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini