Profesa KITILA MKUMBO Ampa Ushauri Huu Edward LOWASSA Kuhusu Matokeo!
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo. Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu. Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi. Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang’anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi. Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo. “Hivyo ...