Mbwa ampiga risasi mmiliki wake

Na katika kisa ambacho kimewaacha watu wengi
kote duniani wamepigwa na butwaa,,,,
Mwanamke mmoja mmiliki wa mbwa huko
Marekani alilazwa hospitalini baada ya jibwa lake
kufyatua bastola na kumjeruhi mguu.
Amini usiamini ni tukio la kweli kabisa.
Afisa wa mazingira wa jimbo la, Indiana,
Jonathon Boyd amenukuliwa akisema kuwa bi
Allie Carter alikuwa ameenda kuwinda bata wa
mwituni akiwa amejihami na bastola yake na
jibwa lake.
''Baada ya muda akawa anahisi amechoka kisha
akaweka bastola yake chini.''
''Kwa bahati mbaya jibwa hilo lilikanyaga bunduki
hiyo na kufyatua risasi iliyomjeruhi bi Carter
mguuni.''
Boyd anasema kuwa bibi huyo alijeruhiwa vidole
vya mguuni lakini amepata matibabu.
Afisa huyo aliongezea kusema kuwa bi Carter
hajakamilisha mafunzo ya msingi kabla
hajaruhusiwa kuwa mwindaji na hivyo akasema
huenda ajali hiyo ingeepukwa ikiwa angekuwa
amekamilisha mafunzo hayo.
Ukistaajabu ya Musa ,,,,,,,
Toa maoni yako kuhusiana na tukio hilo la
kipekee.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini