Nyuma ya Pazia Kampeni za CCM: Mrembo Shombeshombe Amvaa Msanii DIAMOND PLATINUMZ [+PICHAZ]
Richard Bukos
Mambo ya uchaguzi! Ama kweli nyota ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Baba Tiffah’ inazidi kung’aa ambapo Ijumaa iliyopita mrembo mwenye asili ya Kiarabu ‘shombeshombe’ aliwazidi kete mabaunsa wa msanii huyo na kumvaa mzimamzima.
Mambo ya uchaguzi! Ama kweli nyota ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Baba Tiffah’ inazidi kung’aa ambapo Ijumaa iliyopita mrembo mwenye asili ya Kiarabu ‘shombeshombe’ aliwazidi kete mabaunsa wa msanii huyo na kumvaa mzimamzima.
…Akitaka kupiga naye picha.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri wakati Diamond akishuka jukwaani baada ya kuangusha onesho la kusindikiza kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar.
Awali, wakati Diamond akikamua jukwaani, mrembo huyo alionekana kukunwa vilivyo na makamuzi yaliyokuwa yakifanywa na Baba Tiffah ambapo alisikika akimpigia mayowe, ‘Diamooond…I looove youuu… I neeed youuu…Diamond kiiis me now…”
Akiwa katika hali hiyo, mdada huyo hakuna aliyemjali, kila mtu alimuona ni shabiki wa kawaida kabla ya kuzua kizaazaa cha kumganda Diamond.
…Akizi kumng’ang’ania.
Baada ya muda Baba Tiffah alimaliza kufanya shoo na kushuka jukwaani lakini kabla hajashuka vizuri mdada huyo alimvaa mzimamzima na kumkumbatia huku akitaka waachwe wawili.
Kitendo hicho kiliwaamsha mabaunsa waliokuwa wakimlinda mwanamuziki huyo ambao walianza kupambana na mrembo huyo aliyeonekana kuwazidi nguvu na kumtia kwapani Diamond.
Baada ya purukushani kukolea, mdada huyo alizidi kuwaelemea mabaunsa hao huku Diamond naye akionesha sapoti kwa mdada huyo kwa kumkumbatia kimtindo na kuelekea naye kwenye gari alilokuwa ameandaliwa lakini mabaunsa walizidi kumwekea ngumu.
Baada ya kuchomolewa kwa Diamond, mrembo huyo alionekana kuwambembeleza mabaunsa wamuache aongee machache ya moyoni na mwanamuziki huyo lakini aliwekewa uzibe.
Alipoona ameshindwa kabisa, mdada huyo aliishia kuwanung’unikia mabaunsa hao huku akiondoka kwa huruma akigeuka nyuma kumwangalia Diamond kama alimuona.