MADAI MAZITO: Mama KANUMBA Atukanwa na mama LULU!

mamakanumbaaa.jpg 
Mama wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
NA GLADNESS MALLYA
MAMA wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amedai kwamba mama wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresa Kalugira amemtukana matusi mazito yaliyomsababishia presha na vidonda vya tumbo.
MamaLulu.jpg 
Mama wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresa Kalugira.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mama Kanumba alisema wiki mbili zilizopita mama Lulu alimpigia simu usiku wa manane na kuanza kumporomoshea matusi na kumtaka aache kumfuatilia na mwanaye.
“Kweli hayo matusi yameniumiza, mpaka sasa ninaumwa kwani presha inapanda kila nikikumbuka na vidonda vya tumbo hali inayonifanya kila siku niwe ni mtu wa kwenda hospitali tu.
kanumbaAliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Kanumba.
“Inaniuma sana kwani siku hiyo alinitukana matusi ya nguoni, ilikuwa usiku na nahisi alikuwa kalewa, nilipoamka siku iliyofuata nilimtafuta Lulu kwenye simu na kumweleza lakini alirudi upande wa mama yake na kuniambia kama nina uwezo nikashtaki popote.
luluuu
Staa wa Bongo Movie Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Nawashukuru Global Publishers kwa kuona habari kwenye moja ya magazeti yenu kwamba kesi itaanza hivi karibuni, imenipa faraja sana kwani nilikuwa nafikiria kwamba inawezekana hiyo kesi imesahaulika,” alisema mama Kanumba.
Baada ya kupata malalamiko hayo, gazeti hili lilimtafuta mama Lulu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza sina namba ya huyo mama na tangu nimetoka kwenye msiba wa mama yangu sijawasiliana naye, sisi ni watu wazima sasa sijui hata tunagombea nini maana tungekuwa wasichana ningesema labda tunagombea bwana. Anasema nilimtukana, alinirekodi au anazumngumza tu vitu ambavyo havina ushahidi?”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini