UTATA: Unazionaje Kauli Hizi za MAALIM SEIF na Jaji LUBUVA wa NEC Kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar Kufutwa?!
Uchaguzi huu,Vile Vile unaathiri
uchaguzi wa Jamhuri ya
Muungano.Kwamba Wapiga Kura Wa
Zanzibar Wote Walishiriki uchaguzi wa
jamhuri ya muungano.
Lakini anayeendesha Uchaguzi wa
Muungano Hapa (Zanzibar) Ni ZEC
kama wakala wa NEC.
Sasa Ukisema kwamba unafuta
Uchaguzi Zanzibar,Unafuta Uchaguzi wa
RAISI wa jamhuri ya Muungano kwa
upande wa Zanzibar. Unafuta Uchaguzi
wa wabunge kwa upande wa Zanzibar.
Kwa hiyo basi,Huwezi ukamuapisha
raisi atakayechaguliwa kwa upande
mmoja wa Muungano akawa ni Raisi wa
TANZANIA. Na Akiapishwa Huyo
atakuwa ni Raisi wa TANGANYIKA.
Vilevile Huwezi kuwa na Bunge la
Muungano Bila ya Wabunge kutoka
ZANZIBAR. Wakikutana Peke Yao
Itakuwa Ni Bunge La
TANGANYIKA......." ~Maaalim Seif
Sharif Hamad