KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU ZIMEUA SANAA -TIKO Afunguka

Na Gladness Mallya
MWANADADA anayekuja juu katika filamu Bongo, Tiko Hassan amesema kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu zimechangia kuua sanaa ya filamu kwani wasanii wengi walijikuta wakijikita huko na kusahau kazi zao.
 
JUU: Mwanadada anayekuja juu katika filamu Bongo, Tiko Hassan.
 Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Tiko alisema baada ya uchaguzi, wasanii wa filamu wana kazi nzito ya kuirudisha tasnia yao ambayo imefifia kutokana na wengi kujikita kwenye kampeni wakisahau kazi yao.
 “Wanasingizia hakuna soko, lakini hilo siyo tatizo, tatizo ni sisi wasanii kwa sababu hatujui nini tunachotaka hivyo tunatakiwa kubadilika na kujua ni kitu gani tunataka, sanaa imekufa, tuna kazi nzito sana ya kuifufua ili irudi kama zamani,” alisema Tiko.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini