NEC Watoa Tamko Kuhusu Hatima ya Uchaguzi wa Tanzania...UKAWA Nao Watema Cheche!
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva
amesema kuwa kufutwa kwa uchaguzi
mkuu Zanzibar hakutaathiri uchaguzi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa sababu NEC na NEC
wanaongozwa na katiba mbili tofauti.
Lubuva ametoa kauli hiyo leo mchana
ikiwa ni muda mfupi kabla ya
kuendelea na utangazaji wa matokeo ya
Rais.
"NEC inapenda kuwatangazia wananchi
kuwa kuhairishwa kwa uchaguzi
Zanzibar hakutasababisha kuhairishwa
kwa uchaguzi Tanzania.
"Uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa
na ZEC na uchaguzi wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzani unasimamiwa
na NEC, ni katiba mbili tofauti
"Uvumi unaoendelea kwamba uchaguzi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
umefutwa ni upotoshaji na si kweli,
haujaathiriwa na lolote.
"Tuko hapa muda huu kuendelea na
utoaji wa matokeo ya awali kama
ambavyo tumekuwa tukifanya." Alisema
Lubuva na kuendelea na zoezi la
kutangaza matokeo hayo.
Mcheki na Msikilize Jaji Lubuva
akiongea
UKAWA Wapigilia msumari
Akizungumzia sakata la uchaguzi mkuu
kufutwa huko Zanzibar,Mwenyekiti
mwenza wa Ukawa,James Mbatia
amesema kuwa tume ya uchaguzi ZEC
imeamua kuyafuta matokeo hayo baada
ya CCM kushindwa vibaya.
"ZEC wameamua kuufuta uchaguzi
mkuu Zanzibar kwa shinikizo la serikali
ya Kikwete na CCM yake baada ya
Maalim Seif Sharif Hamad kuibuka
kidedea.
"Huwezi kufuta uchaguzi wa Zanzibar
ukaacha uchaguzi wa Jamhuri ya
Muungano
"Unaposema Dola ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa
Katiba ni Tanganyika na Zanzibar
"Upande mmoja wa Jamhuri ya
muungano umefuta uchaguzi, tena
wametamka kufuta uchaguzi mkuu.Sasa
kama upande mmoja umeshafuta,
upande mwingine unasubiri nini?
"Huu ni mgogoro mkubwa. Kitendo cha
Damian Lubuva kuendelea kutangaza
matokeo ni sawa na kiini macho,
anajifurahisha tu mwenyewe na ni
kinyume cha katiba." Amesema James
Mbatia
Mcheki na msikilie Mbatia akiongea