CHADEMA Mtamkumbuka ZITTO KABWE na DK SLAA...CUF Hawataisahau CHADEMA

 
Slaaa 
Kwa mwenendo wa matokeo rasmi viti vya ubunge licha ya CHADEMA kuongeza idadi ya viti hivyo na madiwani  ila bado haijafikia kiwango kile kilichotarajiwa na wengi kwa trend waliyokua wakienda nayo. Hii inaonyesha wazi umahiri wa Zitto kabwe na Dr. Slaa walivyofanya kazi kubwa kwa kutumia upeo wao mkubwa wa ushawishi wa kisiasa kuipa mafanikio makubwa CHADEMA katika uchaguzi uliopita 2010 na kujizolea majimbo mengi ya ubunge na udiwani.

Lakini kama ilivyo chadema ya akina Mbowe ina malengo yake maalumu kwa watu maalumu.na ktk kuelekea kutimiza malengo yake huwatumia wale political genius kama kijiko cha jikoni Kuwavusha point A kwenda point B baadaye huwajengea zengwe ili iwafukuze au waj iengue wenyewe na wakati mwingine huisiwa kutumika hata njia za kimafya ili kuwaweka pembeni kama ilivyo jiri kwa Chacha wangwe, Dr.Kaburu, Zitto kabwe, hatimaye Dr. Slaa hawa kila mmoja alipewa sehemu yake ya kazi na wamiliki wa CHADEMA pasi na wawo kujitambua. wakisaidiwa pembeni na vuvuzela akina Tundulisu na Mnyika. ili kusafisha njia mtoto wao Mbowe aingie Ikulu kirahisi. Kazi hiyo waliifanya na Slaa akawafikisha ktk geti la Ikulu.
 
Zitto Kabwe 
Master plan akaona itakua ni vigumu sana kumuengua slaa kama atafanikiwa kuingia ikulu kwa sababu mzizi wake ktk chama ni wahatari kwa hiyo hapa kuvuka kuingia ikulu lazima apatikane mtu ambaye anaushawishi wa kisiasa lakini hana mzizi ktk chama ili tukisha ingia ikulu iwe rahisi kumuosha kwa bahti isiyotegemewa akapatikana Luwasa tena akawa ni jiwe moja kwa ndege wawili,kwanza ni fimbo ya kumfukuzia Dr,slaa pili ni lift ya kuwaingiza ikulu.tatu kuachia nafasi ni rahisi mno kwa mujibu wa afya yake.

Cuf nawo wakazuguushwa ukuti ukuti bila kujua wakatumika kama petroli ya kuchochea gari la kuipeleka Chadema ikulu bila wawo kutanabahi kuwa kwa mchezo huo baada ya uchaguzi watakufa kifo cha mende mbendembende miguu juu. nafasi yao ya 3 huku bara inachukuliwa na ACT Wazalendo, HEKO ZITTO.

Hii ndio move waliocheza Chadema's master mind. kwa bahati mbaya mkanda umeungua ikulu hakuingiliki na uwakilishi mkubwa wa ubunge na udiwani umetoweka.
Move kama hii Jems hardly chess huiita THE WAY THE COOKIE CRUMBLES. Kwa wale wasomi wa zamani wa novel wanajua.
By Papaayenga/JF

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini