Wananchi Moshi washambulia gari la Kampeni Meneja



Gari hilo aina ya Toyota Verosa namba T756 CPB baada ya kuharibiwa vibaya.

Vijana wakionekana kushangilia baada ya kuliharibu gari hilo.

Gari la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya CCM, Dk. Cyrill Chami, limeshambuliwa na kuharibiwa vibaya na wananchi wakilishuku kuwa na kura bandia.

Katika tukio hilo lililotokea saa 10:00 alasiri katika kijiji cha Uru Kitandu, meneja kampeni huyo wa Dk. Chami aitwaye Kizitto George, aliokolewa na Polisi lakini wakati huo akiwa ameumizwa vibaya kwa kipigo hicho.

Gari hilo aina ya Toyota Verosa namba T756 CPB liliharibiwa vibaya kwa kuvunjwa vunjwa vioo, kung’olewa magurudumu yake, kuibiwa redio ya gari na vifaa mbalimbali kung’ofolewa.

Katibu wa zamani wa Mbunge Chami, Martin Mallya alilithibitishia gazeti hili kutokea kwa tukio hilo akisema gari hilo halikuwa limebeba kura yoyote ila kinachoonekana walikuwa wakimwinda muda mrefu. “Hivi ninavyoongea na wewe niko hapa Polisi majengo ili kufuatilia nijue amepelekwa hospitali gani ila nimeambiwa gari limeharibiwa vibaya,” alisema Mallya ambaye aliwahi kuwa Diwani wa kata ya Okaoni Kibosho kwa tiketi ya CCM.

CREDIT: Mwananchi

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini