Nani Yupo Nyuma ya Kura Fake Uchaguzi Huu?

Ukijiuliza utapata majibu. Nani
amekuwa nyuma ya kura fake ambazo
zimekuwa zikikamatwa kipindi cha
uchaguzi? Je Usalama wa Taifa hawajui
kabisa ni nani ambaye amehusika na
"USHENZI" huo? Hivi Rais Kikwete hajui
lolote kuhusu kura hizo ambazo zote
zilizokamatwa zimeonekana kumpigia
Pombe Magufuli? Tukisema kuwa
Serikali ya Kikwete ndiyo imehusika na
ushetani huo tutakuwa tumekosea wapi?
Ni kura ngapi ambazo zilifanikiwa
kuingia kwenye masanduku na hivyo
kuwakosesha wananchi haki yao ya
kidemokrasia? Kama Serikali hii
haihusiki mbona iko kimya kwenye
kukanusha hilo?
Mwanafunzi mwenye uhakika na somo
analokwenda kufanyia mtihani huwa
haingii kwenye chumba cha mtihani
akiwa na "majibu fake"! Viongozi fake
watazidi kulifanya Taifa letu liwe fake
na kuzidi kudharauliwa na mataifa
mengine jirani. Tuna kila rasilimali ya
kutupa mafanikio lakini kwa kuwa
watawala hawana "akili sahihi" ndiyo
maana tunazidi kushindwa kama Taifa
katika mitihani ya maisha. Nawaza ni
nani aliyekuwa nyuma ya kura fake? Je,
kweli tumekuwa na uchaguzi huru na
wa haki?

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini