TEGETE, Makomandoo YANGA SC Wavurugana, CHUJI Aingilia!

tegete
Mshambuliaji wa Mwadui FC, Jerry Tegete
 Johnson James, Shinyanga
KATIKA kile kilichoonekana ni imani fulani, ‘makomandoo’ wa Yanga, juzi walimzuia mshambuliaji wa Mwadui FC, Jerry Tegete, kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya Yanga kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.
Tukio hilo lilitokea saa 9:00 alasiri kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya timu hizo.


Yanga ndio walikuwa wa kwanza kufika uwanjani hapo, muda mfupi baadaye Mwadui walifika, Tegete ambaye ni strika wa zamani wa Yanga, alikuwa wa kwanza kushuka kwenye gari na akataka kuingia kwenye vyumba vya wapinzani wake hao ili kuwasalimia lakini walinzi hao wakamzuia.
Kutokana na kuzuiwa huko kulitokea mvutano kati ya Tegete na walinzi hao ambapo baadaye uliingiliwa na kiungo wa Mwadui, Athuman Idd ‘Chuji’, lakini muda mfupi baadaye wachezaji hao waliondoka na kuingia kwenye vyumba vyao.

Akizungumza na Championi Ijumaa, shabiki maarufu wa Yanga aliyekuwepo uwanjani hapo, Ally Yanga, alisema: “Hatukumzuia kwa imani za kishirikina lakini tulifanya hivyo ili kumtoa mchezoni kwa kuwa tunajua uwezo wa Tegete.”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini