KWISHNEI! Baada ya Kampeni Kuisha...WEMA SEPETU, BATULI Kwisha Kazi!
Habari kutokwa kwa mnyetishaji wetu wa kuaminika zilieleza kuwa, hali imekuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwani kila wakati walikuwa pamoja huku wakivaa sare lakini sasa hakuna tena kitu kama hicho.
Baada ya kutonywa ubuyu huo, gazeti hili lilimtafuta Wema ambapo alifunguka: “Watu wanapenda kuniona nikiongozana na mtu wakati wote, jambo ambalo si rahisi. Mimi naona tupo sawa na hakuna kitu chochote kati yetu,” alisema Wema.