Tafadhali Mheshimiwa LOWASSA Chukua MAAMUZI Haya Kwa Maslahi ya Watu Wako
Kitu ambacho mmejaribu kukifanya jana ni kuchochea hisia za walioumizwa. Ni jaribio la kutaka kuwapa uhalali wa kuwa na Serikali Mbili - Rais Lowassa (ambaye naye kajitangaza mshindi) na Rais Magufuli ambaye amechaguliwa na Watanzania. Ulipojiunga CHADEMA ulikuwa na uhakika wa kushinda; ulipoona nyomi za watu kukuita "Rais, Rais" uliziamini na sasa unafikiri/unaamini/unadhani kuwa hawa watakuja mitaani kukutetea tena na kukuingiza Ikulu kwa nguvu.
Bw. Lowassa mmependekeza mabadiliko yenu, mkayauza kwa wananchi, na mkaamini wananchi wameyakubali kwa vile walikuja kuyaangalia na kuyafurahia kwani yanaonekana kuyapendeza. Mlipoweka bei yake Watanzania wakakataa kununua. Bila ya shaka wapo walionunua kwa kiasi chao lakini wengi wamekataa. Hata kama kwa kufanya hivyo ina maana ile hela yao ya ada inabidi wailinde.
Tafadhali Lowassa kubali kuwa mshindani mzuri maana sasa rekodi yako katika haya mambo ya kushindana katika demokrasia inaanza kutisha. Utabakia na heshima yako na kwa kwa kweli - kama nitakavyoonesha baada ya vumbi kutulia - nafasi yako katika historia ya siasa za Tanzania imebadilika kwa uzuri kufuatia ushindani huu wa 2015. Yote unayoyalalamikia na kuyaona hayakwenda sawa leo wenzio yalitusumbua kichwa 2010 (kama hukufuatilia). Hakuna dai lolote ambalo mmelidai leo ambalo hatukulidai 2010. HAKUNA.
Hivyo, hairisha kwenda kuchunga, kaa na viongozi wapya wa CHADEMA (kwani Mbowe na wenzie watajiuzulu kufuatia kushindwa kwao katika sanduku la kura) na kuipanga upya CHADEMA mliyoivuruga kweli kweli. Haitokuwa sawa (fair) baada ya yote haya halafu uwakimbie urudi kuchunga (kitu ambacho sidhani kama ulimaanisha hasa). Saidia kuujenga upinzani huu na kuhakikisha mifumo ambayo imekuwa ikitusumbua inavunjiliwa sasa kabla ya 2020. Umeamua kuwa mpinzani, ishi kama mpinzani.
Tafadhali Lowassa.