TAARIFA Kamili Kuhusu Matokeo ya Ubunge na Udiwani Jimbo la NYAMAGANA, Mwanza

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Stanslaus Mabula ametangazwa
mshindi wa mbio za ubunge katika
jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza
kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya
mbunge anayemaliza muda wake,
Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura
79, 280.
Akitangaza matokeo hayo usiku wa
kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi
wa Jimbo la Nyamagana, Peter Mainya,
amesema jumla ya wagombea saba
walichuana kuwania nafsi hiyo ya
kuwawakilisha wananchi wa
Nyamagana.
Mainya amesema, ushindi wa Mabula
umetokana na msingi uliowekwa na
chama chake katika matokeo ya
uchaguzi wa udiwani ambapo kati ya
Kata 18 zinazounda jimbo hilo, CCM
imeweza kujinyakulia Kata 14 huku
Kata nne zikichukuliwa na Chadema.
“Kutokana na msingi huo, Stanslaus
Mabula ameweza kupata kura 81,170.
Hivyo basi, kwa mamlaka niliyopewa,
namtangaza Stanslaus Mabula kuwa
ndiye mshindi wa kiti cha ubunge
katika jimbo la Nyamagana” alisema
Peter Mainya.
Ezekiel Wenje anakuwa mbunge wa pili
wa upinzani kupoteza kiti chake jijini
Mwanza baada ya Highness Kiwia
aliyekuwa anatetea kiti chake cha
ubunge katika jimbo la Ilemela
kuangushwa na Anjela Mabula katika
matokeo yanayoashiria kurejea kwa
utawala wa CCM katika siasa za
Mwanza.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini