"Hatujaridhia kumuachia Maalim Seif kutangazwa mshindi wa Zanzibar" yasema CCM
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha taarifa iliyosambazwa kupitia mitandao ya kijamii ya kuridhia Mgombea wa Chama Cha (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad atangazwe kuwa Rais wa Zanzibar. Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kisiwandui mjini hapa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema wamepokea kwa msikitiko makubwa taarifa hizo alizoziita za uzushi. Alisema chama chake hakipo tayari kuvunja katiba wala sheria kwa kuridhia kuwa Maalim Seif atangazwe, kwani uchaguzi uliofanyika tayari umefutwa rasmi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupitia Gazeti la Serikali. "Mtandao huo wa kijamii ulidai kuwa mimi Naibu Katibu Mkuu niliwataka wananchama na wananchi wote kuridhia hatua hiyo iliyofikiwa ya chama chetu kuridhia kuapishwa Maalim Seif, huku nikisisitiza kwa kuwataka wananchi wote wajitokeze kwa wingi katika sherehe za kuapishwa rais", alisema Vuai. Aliongezea kusema, "mbali ya hayo pia tarifa hizo zilin...