Serikali Yasema Desemba 9 Siyo Siku ya Kazi Kwa Watumishi wa Umma

1.Mkurungezi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene (kushoto) akizungumza mbele ya wanahabari.Kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wake, Vincent Tiganya.Mkurungezi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene (kushoto) akizungumza mbele ya wanahabari.  Kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wake, Vincent Tiganya.

2.Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.3.Mwambene (kushoto) akisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
Mwambene (kushoto) akisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
 SERIKALI imesema  siku ya  Desemba 9 iliyopangwa kuwa siku ya usafi wa mazingira haitawafanya wafanyakazi wa utumishi wa umma kwenda kazini bali wataungana na wananchi kwenye maeneo wanayoishi kwa kufanya usafi wa mazingira. 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwa kwa mujibu wa tamko la Rais Dk. John Magufuli,  siku hiyo itumike kufanya usafi hivyo itakuwa siyo siku ya kwenda kazini. 

Amesema anatambua kuwa kila mwananchi au mtumishi wa umma anayo sehemu anayoishi katika kijiji, kata, wilaya na hata mkoa, hivyo atapangiwa maelekezo ya kusafisha eneo husika kupitia viongozi wa serikali za mtaa husika. 

Amesema kuwa viongozi wa serikali za mitaa wanaendelea  kupewa maelekezo ya kuainisha maeneo ambayo yamekithiri kwa uchafu ili  siku hiyo kuhakikisha yanasafishwa.
Amebainisha  taarifa zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii ya kuwa wafanyakazi wa utumishi wa umma wataenda kazini siku hiyo si za kweli bali ni kutaka kupotosha umma.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini