Pluijm wa YANGA SC Ampoteza Mbaya Kerr wa SIMBA SC

pluijmHans van Der Pluijm.
 Sweetbert Lukonge na Nicodemus Jonas KUFURU ya mkwanja! Wakati Yanga wakitamba kuwa wababe wa makombe kwenye Ligi Kuu Tanzania, lakini katika sekta nyingine wakubali tu yaishe maana Azam inaonekana kuwa kiboko yao katika suala zima la mishahara kuanzia ya wachezaji hadi kocha.

Utafiti wa Championi juu ya makocha wa kigeni hasa Wazungu, umebaini kuwa Muingereza, Stewart Hall wa Azam ndiye kinara wa mkwanja kwa makocha 16 wa timu za Ligi Kuu Bara msimu huu, akidaiwa kukunja kitita cha dola 12,000, sawa na Sh milioni 24 kwa mwezi. Mshahara wake ni sawa na fowadi wake anayeliliwa na Yanga kila asubuhi, Kipre Tchetche.

Katika kuonyesha Azam ina jeuri ya fedha, mshahara wa Hall ni mara mbili ya ule anaopokea Mdachi, Hans van Der Pluijm wa Yanga anayedaiwa kuingiza kitita cha Sh milioni 12 kwa mwezi.

Ni kama utani lakini ukweli ni kwamba nafasi ya tatu inashikwa na Mfinland wa Majimaji, Mika Lonnstrom anayekunja kitita cha Sh milioni 11, akimpiku Muingereza wa Simba, Dylan Kerr. Kerr anaingiza kitita cha dola 5,000 sawa na Sh milioni 10, akiwa sawa na Mfaransa wa Stand United, Patrick Liewing anayedaiwa kuweka kibondoni kiasi hicho.

Kwa makocha wazawa, Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar anaingiza Sh milioni 1.3, kiasi kinachotajwa kuwa kikubwa na miongoni mwa makocha wanaolipwa vizuri, kikiwa ni pungufu ya milioni 8.7 za Mzungu mwenye mshahara kiduchu Bongo hii.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini