Papa Francis: Dini Isitumiwe Kuvuruga Amani!

Misa Kenya (4)Kiongozi wa Wakatoliki duniani, Papa Francis wakati akiwasili katika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi 
Misa Kenya (8)Viongozi wa kanisa Katoliki wakiingia kwenye ibada.
Misa Kenya (1)Papa Francis akiendesha misa.
Misa Kenya (12)…Akiongea na wananchi wakati wa misa hiyo (hawapo pichani).
Misa Kenya (2) Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (wa nne kutoka kulia mbele) akiwa katika misa hiyo.
PAPA Francis wa Kwanza ameongoza ibada ya misa ya kwanza leo barani Afrika akiwa nchini Kenya ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi akisisitiza umuhimu wa kuheshimu familia katika jamii.
Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga amani kwani “Mungu ni Mungu wa amani. 

“Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la dini, kupandikiza woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
“Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguse mioyo ya wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu.”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini