Nakuja SIMBA SC Kuipa Ubingwa -KIONGERA
Martha Mboma Dar es Salaam STRAIKA wa Simba, Mkenya, Paul Kiongera, amesema amefurahi kuona klabu hiyo inathamini mchango wake na ameapa kupiga kazi ili kuhakikisha anaipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Kiongera ambaye alisajiliwa na Simba msimu uliopita, alishindwa kudumu kikosini hapo kutokana na kukumbwa na majeraha ya goti ndipo akatolewa kwa mkopo katika timu ya KCB ya Kenya aliyokuwa akiitumikia kabla ya kutua Simba.
Taarifa zilizopo kwa sasa, tayari mabosi wa Simba wameshakamilisha zoezi zima la kumrudisha straika huyo na anasubiriwa amalize majukumu ya timu yake ya taifa ya Kenya inayoshiriki michuano ya Chalenji nchini Ethiopia ili aungane na wenzake.
“Mpaka sasa mimi ni mchezaji wa Simba kwani nina mkataba nao, lakini walinitoa kwa mkopo kutokana na matatizo ya majeraha niliyoyapata, mkataba wangu unamalizika Juni, mwakani.
“Kwa kweli nimefurahi kusikia kwamba Simba inanirudisha kikosini kwao, kwa kushirikiana na wachezaji nitakaowakuta naamini tutafanya vizuri ikiwemo kupambana na timu nyingine kama Azam na Yanga ambazo ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba. Nataka kuhakikisha kwa kushirikiana na wenzangu, tunaipa timu ubingwa wa ligi mwisho wa msimu huu,” alisema Kiongera.