Msichana Atupwa Jela Baada ya Kumtukana Mwenzake Huko Arusha..Yafahamu MATUSI Hayo Nawe Ujihadhari Hapa...

Mkazi wa Ngulelo, Arusha  Neema Obedi amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kumtukana Zubeda Efasi kuwa ni mgumba, hana kizazi na alichonacho hakina faida, hivyo angemwazima chake ili apate watoto.
 Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu Smathon  Joseph wa mahakama ya mwanzo ya Maromboso Mkoani Arusha. 

Hakimu alisema mshtakiwa huyo alimfuata mlalamikaji na kumtolea matusi hayo huku akijua ni kinyume na sharia na  kutakiwa kwenda jela miezi sita na kulipa faini ya shilingi 300,000.
“Matusi hayafai mbele ya jamii, hii ni aibu kutoa maneno mazito kama hayo kw akuwa sote tumetokana na mwanamke, hivyo anapaswa kuheshimiwa na haipendezi kutoa maneno mazito kama hayo”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini