Mpambe wa LOWASSA 'Apigwa Chini' Chuo Kikuu cha Dodoma

BALOZI Dk. Agustine Mahiga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutokana na aliyekuwa ameshika nafasi hiyo Balozi Juma Mwapachu kumaliza muda wake.



Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alitoa kauli hiyo leo alipozungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mahafari ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 na 27 mwaka huu.



Amesema kuwa Balozi Mwapachu amemaliza muda wake tangu Oktoba 30 mwaka huu.



Aidha amesema kuwa Balozi Mahiga ni mzoefu katika utumishi na amefanya kazi nzuri nje na ndani ya nchi huku akiwa na matumaini makubwa kwamba ataliongoza baraza hilo bila hofu yeyote.



Hata hivyo amesema Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amemuongezea muda wa miezi sita, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Shaban Mlacha ambaye alipaswa amalize muda wake Desemba 30, mwaka huu.



Amesema, uamuzi wa kumuongezea

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini