Kutana na Top 6 ya Mastaa wa Soka Wenye Hasira Zaidi Uwanjani Duniani (+VIDEO)


Moja kati ya michezo inayoongoza kwa kuchukua headlines duniani ni mchezo wa soka ambao nchi nyingi ndio mchezo wanaoupa kipaumbele kuliko michezo mingine, huu ni mchezo ambao una headlines ya rekodi kibao ila leo November 28 naomba nikusogezee Top 6 ya wachezaji wa soka wanaotajwa kuwa na hasira zaidi. 

6- Diego Costa ni mkali wa soka anayekipiga katika klabu ya Chelsea ya Uingereza ila ni moja kati ya wachezaji wenye hasira zaidi uwanjani hususani pale inapotokea kachezewa faulo kwa bahati mbaya na mchezaji wa timu pinzani basi huwa hayaishi kirahisi uwanjani. 

Diego Costa akioneshwa kadi ya njano 
5- Zlatan Ibrahimoic ni staa wa soka kutokea Sweden lakini anakipiga katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ana headlines kadhaa ila ya ukorofi na kubishana na refa hiyo pia ni moja kati ya sifa zake, huwa anatajwa kupaniki pale anapochezewa faulo. 

Zlatan Ibrahimovic 
4- Gennaro Gattuso alikuwa anakipiga katika klabu ya AC Milan na baadae Sion ila ana headlines kadhaa za kuoneshwa kadi kutokana na utamaduni wake wa kujibizana na marefa pale ambapo anapokuwa anapingana na maamuzi yao uwanjani haoni hasari kumfokea refa au mchezaji wa timu pinzani pale tu anapokuwa hajaridhdishwa na tukio fulani. 

Gennaro Gattuso akimkaba kocha msaidizi wa Spurs hii ilikuwa ni mechi kati ya Spurs dhidi ya AC Milan ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 
3- Roy Keane huyu ni kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza ambaye amewahi kutamba sana kwa umahiri wake katika nafasi ya kiungo, ukitaja wachezaji wenye hasira katika soka hakika huyu huwezi kumkosa, kwa sasa amestaafu soka. 

Roy Keane akizozana na muamuzi 
2- Oliver Khan ni golikipa wa Ujerumani amecheza timu ya taifa na amewahi kuitumikia klabu ya FC Bayern Munich lakini ni moja kati ya magolikipa bora waliowahi kuitumikia Bayern na Ujerumani. yupo nafasi ya pili katika list ya wachezaji wenye hasira uwanjani. 

Oliver Khan 
1- Pepe ni beki wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania, ukorofi na matukio yake anayofanya uwanjani yamefanya kuwa anaoneshwa kadi nyekundu mara kwa mara uwanjani, sio aina ya mchezaji ambaye atavumilia jambo lisilomfurahisha lipite lakini ni mchezaji anayependa kufanya faulo za makusudi uwanjani. 

Pepe akioneshwa kadi nyekundu kwa makosa yake ya uwanjani. 

Hili ni moja kati ya matukio ya Pepe uwanjani, alimkanyaga Lionel Messi katika mchezo wa El Clasico. 

Hii ni video ya matukio ya mastaa wote sita wenye hasira uwanjani

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini