Wafuasi wa Chadema wafutiwa kesi ya unyang’anyi wa silaha

Wafuasi wa Chadema katika moja ya mikutano ya
Wafuasi wa Chadema katika moja ya mikutano ya chama hicho. Picha na Maktaba
By Christopher Maregesi, Mwananchi
Bunda. Mahakama ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara,
imewafutia kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha wafuasi
watatu wa Chadema baada ya kukosa ushahidi wa kuwatia
hatiani.
Waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo ni Gregory Juma (29), mkazi wa Mkuyuni mkoani Mwanza, Ibrahim Issa (20), wa Saranga Bunda na Lucas Andrea (30),
wa Area A mkoani Dodoma.
Hakimu Ahmed Kasonso alisema licha ya upande wa mashtaka kupeleka mashahidi wanne mahakamani hapo ni mmoja aliyetoa maelezo yanayoendana na kesi hiyo.
Alisema hali hiyo hailipi uzito wa kisheria shauri hilo kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo
bali inatoa mwanya wa kuliondoa hivyo washtakiwa watabaki na shtaka moja la wizi wa simu.
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Septemba 28 wakidaiwa
kumteka kisha kumpora simu mbili na Sh35,000 Charles Yapanda, ambaye ni Katibu wa CCM
Kata ya Kunzugu wilayani hapa huku wakimtishia kwa silaha.
Hata hivyo, kipindi chote cha shauri hilo, Wakili Peter Mwakolo anayewatetea washtakiwa
alikuwa akiiomba mahakama kufutwa kwa madai kuwa limejengwa katika misingi ya kisiasa na

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini