Hili la Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kufuta Likizo ni Kuweka Watu Vizuizini ni Ukiukwaji wa Sheria!

Siungi mkono na sitothubutu kuunga mkono matamko ya wakuu wa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kufuta likizo za watumishi wa umma kwa mwezi huu wa December bila kutolewa ufafanuzi wa kisheria! Hizi ni dalili za utawala wa kimabavu na usiotumia weledi na maadili ya kazi! Likizo za watumishi wote wa umma zipo kwa mujibu wa sheria! Mfanyakazi yeyote yule wa umma aliyeajiriwa na anayelipa kodi serikalini ana haki ya msingi kabisa ya kupata likizo ya siku 28 kwa kila mwaka wa utumishi! Hata waalimu huwa hawaendi likizo pale ambapo wanafunzi wamefunga shule! Wao huwa na likizo zao ambazo zipo kwa mujibu wa sheria!

Mkuu wa wilaya kuweka watumishi wa umma kifungoni bila kuwa na maelezo yoyote ya kuridhisha ni dalili za utawala wa kimabavu hatuongozi nchi kwa "Presidential decree" Kiasi kwamba kila kiongozi anaweza kufanya maamuzi kwa kutamka tu na kisha akawa haojiwi! Kumuweka mtu korokoroni ni lazima kuna kosa na ni lazima mahakama iamue haki! Huwezi kumfunga mtu kwa muda kadhaa bila kuwepo na maelezo yoyote kisheria! Mahakama ina kazi gani?

Kumekuwa na tabia zinazoenda kinyume kabisa na maadili ya utumishi wa umma za viongozi kutoa matamko kandamizi na yasiyofuata taratibu za utawala bora kwa lengo tu na wao waonekane wamo kwenye list ya machachari! Waonekane kuwa na wao wamo!

Tunatakiwa watu wajitume ndiyo, tunataka watu wawajibike ndiyo! Lakini tusifanye hivyo kwa kutumia mfumo kandamizi ambao naona unahasisiwa ndani ya Taifa! Hatupo tayari kuona hilo! Watu wafuate taratibu, kanuni na maadili ya utumishi wa umma!

Enzi za utawala wa Kikwete kuna D.C aliwahi kuwachapa waalimu viboko na watu wakapaaza sauti! Nadhani tusipokemea haya kuna wengine watafanya hivyo na kwa hurka ya utawala wa sasa huenda wakaungwa mkono! Ni lazima tujue kuwa sisi tumeshakubali kuwa nchi ya kidemokrasia na nilazima tufuate kanuni za utawala huo!

Tumeona Zanzibar mtu anafuta uchaguzi kinyume kabisa na taratibu watu wanaunga mkono! Hizo ni dalili za utawala mbovu kabisa! Naomba ieleweke kuwa siungi mkono wizi wala uzembe kazini ila katika kuwajibishana ni lazima zitumike kanuni na sheria halali!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini