Abiria Wamepona Kwenye Ajali ya Ndege na Bado Wanafungua Kesi ya Ajali..

Ikitokea unakuwa sehemu ya watu walionusurika kwenye ajali, jambo kubwa ambalo wengi wanaanza nalo ni kumshukuru MUNGU kwa kutoka salama !!
Kama uko karibu na headlines za stori za kimataifa najua utakumbuka ile ajali ya ndege yaBritish Airways iliyotokea uwanja wa ndege  Las Vegas Marekani wakati ndege ikijiandaa kupaa.
Taarifa nyingine toka Chicago Marekani inahusu kesi ambayo imefunguliwa kuzishtaki Kampuni mbili, GE Aviation watengenezaji wa engine ya ndege iliyopata ajali, pamoja naBoeing Company ambao ndio watengezaji wa ndege yenyewe.
777 Everett Factory K65682-02
Abiria hao 65 waliofungua kesi hiyo wamesema wanazishtaki Kampuni hizo kwa sababu walipata misukosuko wakati wa ajali hiyo ambayo ndege waliyopanda ililipuka na kushika moto kwenye engine yake moja wakati ikiwa kwenye njia ya kurukia ndege uwanja wa McCarran International Airport, September 8 2015.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini