WEMA SEPETU Kiboko Aiseee!


Zuber Shabani akiwa na mama yake getini kwa Wema Sepetu.
Imelda Mtema
Wema kiboko! Dogo ambaye anadai yeye ni chipukizi wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuber Shabani ametoa kali ya mwaka baada ya kutishia kujiua kwa kukosa kupata nafasi ya kuonana na Wema Isaac Sepetu kwa ajili ya kumsaidia shida zake mbalimbali.
CHANZO CHA HABARI
Ijumaa iliyopita, chanzo kimoja cha habari kilipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kutonya kuwa, takriban siku kumi na tano sasa, mama na mwanaye huyo wamekuwa wakifika asubuhi na mapema getini kwa Wema na wanashinda hapo kwa siku nzima lengo likiwa mtoto huyo kumwona Wema.

Wema Sepetu.
MSOSI WA MCHANA GETINI
“Mbaya zaidi, Wema akitoka au akiingia anawachunia. Anajifanya yupo bize hivyo wao wanaendelea kukaa palepale getini. Ikifika mchana, wanakwenda kununua chipsi na kurudi kuzila palepale,” kilisema chanzo.


WIKIENDA LAWEKA MTEGO
Baada ya gazeti hili kuinyaka ‘nyuzi’ hiyo na kuambiwa hata muda huo, mama huyo na mwanaye wapo getini, paparazi wetu alikanyaga njia hadi nyumbani kwa Wema, Makumbusho, Dar ambapo kweli aliwakuta wawili hao na kufanya nao maohijano.
Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Chetu Omar alisema mwanaye ana nyimbo zake anataka kusaidiwa kuingia studio, ndiyo kisa cha kumsaka Wema kwa siku hizo zote.
Kijana kwa Wema (2)
“Mimi nilichukua jukumu la kuja naye ajionee mwenyewe kwa sababu nilihisi kama anaona sifanyi jitihadi za kumtafuta huyo Wema. Kila siku tunatoka Kawe kuja hapa. Katika siku tulizokuja tulijua lazima tungemuona Wema lakini bado hatujafanikiwa. Kinacholeta shida, mwanangu anatishia kujinyonga kama Wema atamkatalia,” alisema mama huyo.
Kijana kwa Wema (3)MTOTO SASA
Kwa upande wake, mtoto huyo alisema kuwa hata kama itachukua muda wa miezi sita, sawa tu! Shida yake kukutana uso kwa uso na Wema na anajua akimsikiliza tu atampa nafasi ya kurekodi naye.
“Mimi najua Wema akiniona na kunisikiliza atanipa nafasi tu ya kufanya naye video yangu,” alisema kijana huyo.


WEMA NAYE
Baada ya kuona mshangao huo, gazeti hili lilimtafuta Wema ambapo alisema kuwa pale kwake wanafika watu mbalimbali hivyo si rahisi kujua kama ndiyo hao au la! Maana anakutana na watu wengi.
“Mimi kwa kweli naonana na watu tofautitofauti sana wakija hapa kwangu. Sasa si rahisi kujua kama ni wao au la!” alisema Wema

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini