Watu wanne wahukumiwa jela miaka 32 Nzega

Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega imewahukumu kifungo cha miaka 32 jela watu nane kwa kosa la kufanya uvamizi na kuiba dhahabu tofali sita na nusu zenye thamani ya zaidi ya hsilingi bilioni 4 katika mgodi wa dhahabu wa resolute
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi silyvester kainda amesema washitakiwa mawazo saliboko ,edward bunera ,shaaban amuru,john ndaki,pius shija ,aloyce zindoro ,davidi ndaki pamoja na frenk kabuche wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada kutiwa hatiani kwa makosa mawili
makosa hayo ni kula njama za kufanya uhalifu katika mgodi wa dhahabu wa resolute ambalo wamehukumiwa kwenda jela miaka miwili kila mmoja pamoja na kosa la pili kufanya uhalifu kwa kutumia silaha ambapo ambalo wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja.
Watuhumiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa 16 likiwepo kosa la kula njama ya kufanya uhalifu,kufanya uhalifu kwa kutumia silaha na utakatishaji pesa haramu.
Akisoma mashitaka hayo mwanasheria wa serikali pius hilla aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo mwezi mei mwaka 2009 watuhumiwa hao walikula njama na kuvamia mgodi wa dhahabu wa resolute uliopo wilayani nzega na kufanikiwa kupora dhahabu matofali sita na nusu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini