MAGUFULI Azidi Kuwaweka Watendaji wa Serekali Roho Juu!

Katika kile kinachoonekana ni kutaka kwenda na kasi ya rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rada kata ya Majohe, Jimbo la Ukonga, Abdallah Goma, amewatimua ofisini wajumbe watano wa mtaa na kuwataka waende mitaani kukusanya kero zinazowakabili  wananchi.

Mwenyekiti huyo aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya  wananchi kulalamikia tabia ya wajumbe  hao kuwadai  malipo  wakati  wanapokwenda kutaka huduma katika ofisi hiyo, ikiwamo kuandikiwa barua ya utambulisho benki.

Goma aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam  jana kutokana na mvutano uliojitokeza  kati yake na wajumbe aliowatimua kugoma kutekeleza agizo lake na kususia vikao.

Alisema  baada ya kuapishwa alipanga ratiba ya kila mjumbe kukaa ofisini kwa muda wa siku mbili, lengo likiwa ni kubaini tabia zao, hivyo katika kipindi hicho malalamiko ya lugha chafu, kudai malipo ya kuandika barua ya dhamana na utambulisho yalijitokeza. Tumeamua kutoa huduma  bure  au kwa kuchangia  gharama kidogo ya uchapishaji lakini siyo lazima ikiwa  mwananchi  hawezi  kuchangia, alisema. Alisema wajumbe waliruhusiwa kukaa ofisini kabla ya serikali kuajiri  Afisa Mtendaji wa Mtaa, lakini  kwasababu mtendaji ameshaajiriwa kazi ya wajumbe hao ni kukusanya kero tu.
Mmoja wa wajumbe hao, Siwema Makamba, alisema  wao wanajitambua kuwa ni wajumbe halali waliochaguliwa na wananchi na ni wajibu wao kuwatumikia kwa nguvu zao zote.

Alisema kitendo cha Mwenyekiti kuwafukuza ofisini ni kuwadhalilisha  ili  yeye atumie fursa  hiyo kurudisha pesa zake alizotumia kwenye uchaguzi na kwamba  siyo haki kwa wao  kwenda kuzunguka mitaani.

Changamoto ya ofisi ymtaa ni  kutokuwa na  mawasiliano mazuri na kusababisha mvutano wetu na mwenyekiti, tunapaswa kuondoa tafauti ili tufanye kazi za wananchi, alisema.

Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Rada, Maulid Janga alisema  yeye   amesikitishwa na kitendo cha wajumbe  kumlipisha Sh. 50,000 kwa ajili ya kuliinua baraza la mtaa kwenda kushughulikia mgogoro wa mpaka.

Unajua hadi leo mgogoro  wa mpaka haujashughulikiwa  na  pesa  zimeliwa hivi hivi na wajanja,  kama walijua hawawezi kutatua tatizo kwanini wachukue fedha zangu, alisema kwa masikitiko.

Afisa Mtendaji wa kata ya Majohe Serrda Chidaga,  alisema yeye ameshangazwa  na  mvutano  wa  wajumbe  kungíangíania  kukaa ofisini na kushindwa kwenda mtaani kukusanya kero za wananchi.Baraza la maendeleo la kata (WDC) limekaa na kujadili suala hilo na kutoa maelekezo kuwa hawatakiwi kukaa ofisini lakini nashangaa bado wanangíangíania,  lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe  ikibainika  kuna  maslahi  binafsi,î alisema.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini